Asante kwa kufungua kiungo hiki cha utafiti wa upendeleo wa kijinsia. Utafiti huu ni sehemu ya uchunguzi wa kujifunza – Utafiti wa Kijinsia wa Kibinadamu – uliyofanyika kwenye Kituo cha Matibabu cha Beth Israel Deaconess (BIDMC), kituo cha matibabu cha kitaaluma cha Shule ya Tiba ya Havard iliyoko Boston, Massachusetts, Marekani.

Uchunguzi huu ni juu ya upendeleo wa kijinsia katika sekta ya kibinadamu. Utafiti unahusisha tafiti mbili za idadi ya wataalamu wa kibinadamu duniani. Utafiti huu ni juu ya upendeleo wa kijinsia katika mahali pa kazi na unahusisha maswali kujulisha hatua za baadae. Kuna utafiti mwingine unaolenga unyanyasaji wa kijinsia katika muktadha wa janga la COVID-19 na mwitikio.

Kila utafiti utakuchukua kama dakika 20-30 kumaliza. Unaweza kuchagua kushiriki katika utafiti mmoja au tafiti zote. Kama unapenda kushiriki katika mahojiano ya mtu binafsi au majadiliano yanayolenga kikundi kama sehemu ya utafiti huu, utakuwa na chaguo la kuonyesha upendeleo wako ili tuwasiliane na wewe.

Tunaomba barua pepe yako ili tuweze kukushirikisha kiungo cha utafiti wa pili na kuwasiliana na wewe kama unapenda kushiriki katika mahojiano au majadiliano yanayolenga kikundi. Barua pepe yako itaondolewa kutoka kwenye takwimu kabla ya uchambuzi kufanyika, hivyo taarifa haitatambulika. Barua pepe yako haitashirikishwa kwa wahusika wa tatu. Tutalinda usiri na usalama wa taarifa zako. Takwimu zitahifadhiwa kwa usalama, na haitawezekana kukutambua wewe katika matokeo yoyote kutoka kwenye uchunguzi huu.

Ushiriki ni wa hiari, na unaweza kusimamisha utafiti muda wowote. Kama mahali popote wakati wa utafiti unaamua kuwa hautaki tena kushiriki, taarifa zako binafsi ambazo zimeshakusanywa tayari hadi muda wa kujitoa kwako zitatunzwa na kutumika

kuhakikisha uadilifu wa utafiti na/au kwa matumizi mengine yoyote yaliyoruhusiwa chini ya sheria za ulindaji takwimu na usiri zinazotumika. Ingawa sio ya faida ya moja kwa moja kwako, matokeo kutoka katika utafiti huu yanaweza kuimarisha upangaji wa baadae wa kibinadamu na kuimarisha usawa wa kijinsia katika mahali pa kazi ya kibinadamu. Haitakugharimu wewe kitu chochote kushiriki katika utafiti. Hautapokea fidia kwa muda wako kumaliza utafiti.

Kama una maswali yoyote au mashaka kuhusu utafiti, unaweza kuwasiliana na Mtafiti Mkuu aliyepo BIDMC [Dr. Jennifer Scott kwa jscott3@bidmc.harvard.edu au +1 617-667-4165]. Kama ungependa kuongea na mtu ambaye hajahusishwa katika utafiti, unaweza kuwasiliana na Ofisi ya Ulindaji Washiriki wa Kibinadamu ya Kituo cha Matibabu cha Beth Israel Deaconess kwa +1 (617) 975-8500.

Asante kwa muda na ushiriki wako!

Page 1 of 12

Loading... Loading...
You have selected an option that triggers this survey to end right now.
To save your responses and end the survey, click the 'End Survey' button below. If you have selected the wrong option by accident and/or wish to return to the survey, click the 'Return and Edit Response' button.